TISEZA YAZINDUA DAWATI LA HUDUMA KWA WAWEKEZAJI SHINYANGA, YAENDESHA SEMINA YA KUHAMASISHA UWEKEZAJI WA NDANI
TISEZA YAZINDUA DAWATI LA HUDUMA KWA WAWEKEZAJI SHINYANGA, YAENDESHA SEMINA YA KUHAMASISHA UWEKEZAJI WA NDANI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, na Meneja wa Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani kutoka TISEZA, Bw. Felix John (kulia), wakikabidhiana nyaraka za kuscan ( QR Codes ) wakati wa uzinduzi wa Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) imezindua rasmi Dawati la Huduma kwa Wawekezaji Mkoa wa Shinyanga, hatua inayolenga kusogeza huduma za uwekezaji karibu zaidi na wananchi, hususan wawekezaji wa ndani na wajasiriamali wa mkoa huo. Uzinduzi huo umefanyika leo Ijumaa, Januari 30, 2026, sambamba na utekelezaji wa semina ya uhamasishaji wa uwekezaji wa ndani iliyowakutanisha wajasiriamali, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali wa sekta ya uwekezaji mkoani Shinyanga. Tukio hilo ni sehemu ya Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji wa Uwekezaji wa Ndani inayoendelea kutekelezwa katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita. K…