Posts

RC SENDIGA APINGA TAKWIMU ZA DAWA MANYARA

RC SENDIGA APINGA TAKWIMU ZA DAWA MANYARA
Na Mwandishi Wetu, Manyara. MKUU wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga, amepinga takwimu zinazoonesha kuwa upatikanaji wa huduma za dawa mkoani humo umefikia asilimia 93, akisema kuwa takwimu hizo haziakisi uhalisia wa hali iliyopo kutokana na wingi wa malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ukosefu wa dawa na huduma muhimu za afya. Sendiga ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kuanza utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote (BAW) ngazi ya mkoa wa Manyara, kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kikihusisha wadau wa afya wakiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa, waganga wakuu wa wilaya pamoja na kamati za afya za halmashauri. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa bima ya afya kwa wote hauwezi kufanikiwa endapo wananchi wataendelea kukumbana na kero za ukosefu wa dawa, vipimo na huduma nyingine muhimu katika vituo vya afya na hospitali. “Huduma bora za afya lazima ziende sambamba na bima ya afya kwa wote. Wananchi hawapaswi kulalamika,” amesema RC Sendiga. Katika kuhakikisha mpango huo u…