NIRC, JKT ZAUNGANA KUONGEZA UZALISHAJI KUPITIA UMWAGILIAJI
NIRC, JKT ZAUNGANA KUONGEZA UZALISHAJI KUPITIA UMWAGILIAJI
📍 Mlimba, Kilombero – Morogoro Shamba la Chita JKT, lenye ukubwa wa ekari 12,000 zinazolimwa, limepangwa kuwa mfano wa ushirikiano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC). Tangu mwaka 2021, Jeshi limekuwa likiendeleza mashamba haya kwa kutumia rasilimali za ndani, likikodisha mitambo na kusawazisha mashamba ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mpunga. Katika ziara yake ya hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Bw. Raymond Mndolwa, ametembelea maeneo ya mito yenye miundombinu ya kupeleka maji mashambani na kukutana na uongozi wa JKT katika skimu hiyo na kutoa maagizo mahsusi ya kuimarisha skimu hiyo na kuahidi kuchukua hatua za haraka ndani ya siku 14, lengo likiwa ni kuijengea uwezo CHITA JKT katika uzalishaji wa mazao. Bw. Mndolwa amesisitiza kuwa upo umuhimu wa kutafuta mbinu ya uhifadhi wa maji, ikiwemo kujenga mabwawa, ili maji mengi yanayopotea yaweze kuhifadhiwa na kutumika kwa Umwagiliaji.Ameeleza “Kunauhitaji wa kujengwa bwaw jipya, lijengwe kwa…