MBUNGE MAVUNDE KUANZISHA KLABU ZA MAMA LISHE KILA KATA JIMBO LA MTUMBA
MBUNGE MAVUNDE KUANZISHA KLABU ZA MAMA LISHE KILA KATA JIMBO LA MTUMBA
▪️Lengo ni kurahisisha upatikanaji wa mitaji na mikopo ▪️Mama Lishe Mtumba kugaiwa mashamba kulima mbogamboga ▪️Majiko 1000 yatolewa kwa Mama Lishe ▪️Mtumba wamuunga mkono Rais Samia juu ya matumizi ya Nishati safi Mbunge wa Jimbo la Mtumba, Mh. Anthony Mavunde kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx leo amekabidhi jumla ya majiko 1,000 ya gesi kwa mama lishe na baba lishe wa Jimbo la Mtumba, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuunga mkono jitahada za Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan katika kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia. Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo, Mavunde amesema mpango huo unalenga kuboresha afya za mama na baba lishe, kuongeza ufanisi katika shughuli zao za kila siku pamoja na kulinda mazingira kwa kupunguza matumizi ya mkaa na kuni. Amesema kuwa Wananchi wa Mtumba kwa kushirikiana Serikali wataendelea kuweka mazingira rafiki kwa wajasiriamali wadogo ikiwemo upatikanaji wa nishati safi kwa makundi mbalimbali ya jamii ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. Mavund…