KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA SAMIA LEGAL AID YAJA KIVINGINE, SASA KUTOKOMEZA KABISA MIGOGORO YA ARDHI

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA SAMIA LEGAL AID YAJA KIVINGINE, SASA KUTOKOMEZA KABISA MIGOGORO YA ARDHI
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha  SERIKALI imesema imejiandaa kutokomeza kabisa migogoro ya ardhi nchini kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni Jijini Tanga na baadae kuendelea katika Mikoa mingine. Akizungumza Jana Januari 30, 2026 Jijini hapa wakati wa kufunga Mafunzo kwa Mawakili wa Serikali kuhusu masuala ya msaada wa kisheria (Mama Samia Legal Aid) katibu Mkuu wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi amesema migogoro ya ardhi imekuwa tatizo kubwa nchini. “ Katika awamu ya kwanza na ya pili ya zoezi la kampeni ya kutoa msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid, migogoro ya ardhi ilionekana kuwa kinara dhidi ya malalamiko mengi yaliyokuwa yakihitaji msaada wa kisheria,” “ Kwa kuwa tumegundua hilo ni tatizo kubwa, Serikali hivi sasa tumejipanga kuhakikisha tunatokomeza kabisa migogoro hii na kufanya watu waishi kwa amani,” amesema. Amesema tofauti na awamu zingine za kampeni hiyo, awamu hii migogoro itakayowasilishwa w…