Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick
Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Barrick Corporation, mwanahisa mwenza wa Twiga Minerals Corporation Limited (TWIGA), pamoja na uongozi wa TWIGA, kujadili maendeleo na masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa miradi inayosimamiwa na kampuni hiyo. Mazungumzo hayo yalifanyika Jumanne, Septemba 1, 2026, wakati ujumbe wa Barrick ulipofanya ziara katika Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), jijini Dar es Salaam. Ujumbe wa Barrick uliongozwa na Roelie Gey Von Pittius, Meneja wa Fedha wa Barrick kwa Afrika na Mashariki ya Kati, akiambatana na Candace Simpson, Meneja wa Kodi wa Afrika na Mashariki ya Kati; Melkiory Ngido, Meneja wa Barrick nchini Tanzania; na Judith Chambua, Meneja wa Kodi wa Barrick Tanzania. Katika kikao hicho, Serikali, kupitia OTR, na Barrick, ambao ni wanahisa wenza wa TWIGA, walijadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo na uendeshaji wa miradi ya uchimbaji wa dhahabu inayomiliki…