DCEA YAZINDUA KLABU KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA VYUO VIKUU,KAMISHINA AFUNGUKA

DCEA YAZINDUA KLABU KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA VYUO VIKUU,KAMISHINA AFUNGUKA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA)imezindua Klabu za kupiga vita dawa za kulevya katika vyuo vikuu nchini ikiwani sehemu ya juhudi za Serikali za kuimarisha ushiriki wa jamii hususani wanafunzi wa vyuo vikuu katika kudhibiti na kupambana na tatizo la dawa za kulevya Hatua ambayo pia inalenga kuimarisha kinga, kuongeza uelewa na kujenga mazingira yatakayosaidia vijana kufanya maamuzi salama na yenye tija kwa mustakabali wa maisha yao na Taifa kwa ujumla. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa klabu hizo leo Septemba 1,2026 katika ukumbi wa Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ,Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo Aretas Lyimo amesema vilabu hivyo vitatumika pia kutafakari kwa mtizamo wa kitaaluma kuhusu tatizo la dawa za kulevya. Pia athari zake kwa vijana wa kizazi kipya kwani uraibu ni tatizo linalopoteza utu na kusababisha mateso kwa vijana. “Katika kubabiliana na tatizo hili, kunahitaji majibu ya kina na hatua za uzuiaji zinazohusish…