ZIARA YA RAIS SAMIA URUSI YAFUNGUA FURSA 10 ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA
ZIARA YA RAIS SAMIA URUSI YAFUNGUA FURSA 10 ZA UFADHILI WA MASOMO KWA WATANZANIA Na Dotto Kwilasa,Dodoma Ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini Urusi imeanza kuzaa matunda katika sekta ya elimu baada ya Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi (RUDN University) kutoa nafasi 10 za ufadhili wa masomo kwa Watanzania pamoja na kuimarishwa kwa ushirikiano wa kitaaluma kati ya nchi hizo mbili. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, alisema mafanikio hayo yametokana na mazungumzo yaliyofanyika wakati wa ziara ya Rais Samia nchini humo. Alisema moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana ni Rais Samia kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima na RUDN, taasisi inayotambulika kimataifa kwa mchango wake katika elimu, tafiti na ubunifu wa kisayansi. Kwa mujibu wa Prof. Mkenda, kutunukiwa kwa Rais Samia shahada hiyo ni ishara ya kuimarika kwa uhusiano wa Tanzania na Urusi katika sekta ya elimu na kumefungua milango ya ushirikiano mpana zaidi kati ya taasisi za elimu za mataifa hayo. “Chuo kilichomtunuku …