WRRB YANADI UFANISI WA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA MISRI, YAFUNGUA MILANGO YA BIASHARA YA MIFUGO
WRRB YANADI UFANISI WA MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA MISRI, YAFUNGUA MILANGO YA BIASHARA YA MIFUGO Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu, ameshiriki Jukwaa la Tanzania na Misri la Utalii, Biashara na Uwekezaji na kueleza kuwa Tanzania imeongeza biashara ya mifugo na mazao ya mifugo katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kuwa unazingatia uwazi, ubora na uaminifu katika biashara. Akizungumza katika jukwaa hilo (Tanzania–Egypt Tourism, Trade and Investment Forum) lililofanyika nchini Misri na kuwakutanisha wadau wa biashara, uwekezaji na utalii, Bangu amesema mfumo unaotumika kusimamia biashara ya mazao ya kilimo sasa uko tayari kuhudumia pia sekta ya mifugo. Akifafanua ufanisi wa matumizi ya mfumo huo katika moja ya mijadala iliyokuwepo kwenye jukwaa hilo, Bangu amesema wamefanya kikao kifupi na ujumbe wa Misri ambao wameonesha nia kubwa ya kufanya biashara ya mifugo na bidhaa zitokanazo na mifugo kutoka Tanzania. “Tunawakaribisha wafanyabiashara wa Misri kuja kufanya biashara Tanzania. Mfumo wetu wa Stakabadhi za Ghala n…