SHEIKH PEMBE ASISITIZA KUHUSU UMUHIMU WA AMANI, ATAKA WAISLAMU KUILINDA NCHI YAO

SHEIKH PEMBE ASISITIZA KUHUSU UMUHIMU WA AMANI, ATAKA WAISLAMU KUILINDA NCHI YAO
Imamu Mkuu Masjid Mtambani Sheikh Shabani Pembe amewataka Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kudumisha na kuilinda amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa ikiwa serikali ingeruhusu kufanyika kwa kile kilichokuwa kimepangwa, kuratibiwa na kuhamasisha Oktoba 29, 2025 basi Tanzania isingeweza kukalika tena kutokana na uvunjifu wa amani ambao ungetokea wakati ule wa Uchaguzi. Sheikh Shabani Pembe amebainisha hayo wakati akitoa hotuba yake kwa waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dar Es Salaam na kuwataka Waislamu kuhukumu kile kilichotokea kwa uadilifu pamoja na kupima athari ambazo zingeweza kujitokeza ikiwa serikali ingewaaacha wale waliokuwa wamejitokeza barabarani kuendelea na matukio yao ya uvunjifu wa amani Nchini. "Kituo chetu cha mwendokasi tumeshuhudia kikichomwa, Vituo vya Polisi vilichomwa, ATM pale Manyanya imechomwa na hata maduka ya watu yamechomwa na kuibiwa, hawa watu wangeachiwa wafanye wanavyotaka hii Nchi ingekuwa wapi? Ndugu zangu tunapohukumu tuhukumu kwa u…