SAMIA AWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA ASKARI ASIYEFAHAMIKA URUSI

SAMIA AWEKA SHADA LA MAUA KATIKA KABURI LA ASKARI ASIYEFAHAMIKA URUSI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la maua katika Kaburi la Askari Asiyejulikana (Tomb of the Unknown Soldier) pembezoni mwa Ukuta wa Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow nchini Urusi, tarehe 03 Juni, 2026. …………  Na Beda Msimbe, TBN, Moscow Kengele kubwa iliyogongwa mara tisa huku bendi ya jeshi ikiongoza nyimbo za maombolezo, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan majira ya saa tano na dakika 23 aliweka shada la maua katika kaburi la Askari Asiyefahamika mjini Moscow, Urusi. Baada ya shughuli hiyo ya uwekaji wa shada la maua katika eneo ambalo moto huwaka daima kama kumbukumbu ya wapiganaji wa Urusi waliopoteza maisha katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, gadi tatu za heshima zilipita kwa mwendo wa haraka kutoa salamu za heshima kwa Rais Samia, sambamba na kupigwa kwa wimbo wa Taifa wa Tanzania. Nidhamu ya askari waliokuwa katika uwanja huo ilivutia wengi, ambapo walionekana kusimama kwa umakini mkubwa bila kutikisika katika maeneo yao ya ulinzi. Aidha, ubadil…