OFISI YA WAZIRI MKUU NA OMDTZ ZAIMARISHA UTAYARI WA JAMII KUKABILIANA NA MAFURIKO DAR ES SALAAM

OFISI YA WAZIRI MKUU NA OMDTZ ZAIMARISHA UTAYARI WA JAMII KUKABILIANA NA MAFURIKO DAR ES SALAAM
Na, mwandishi wetu - Dar es Salaam Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi OpenMap Development Tanzania (OMDTZ), kupitia mradi wa Ramani Zetu, Sauti Zetu imeendesha warsha ya kupitia na kuthibitisha Mipango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa kata tano za Makurumula, Mabibo, Keko, Ubungo na Tabata jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imewakutanisha viongozi wa serikali za mitaa, Kamati za Usimamizi wa Maafa za Kata, wataalamu wa usimamizi wa maafa, waratibu wa maafa wa mkoa na wilaya pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha mipango hiyo inakidhi mahitaji halisi ya jamii zinazokabiliwa na hatari ya mafuriko Dar es Salaam. Akifungua warsha hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa Operesheni za Maafa kutoka Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Kanali Selestine Masalamado amesema kuwa ubora wa mpango wa maafa hupimwa kwa uwezo wake wa kutekelezeka na kuleta matokeo chanya kwa wananchi, huku akisisitiza umuhimu wa mipango hiyo kuzi…