DAWASA, JIJI, TARURA WAZIBUA MITARO YA MAJI TAKA INAYOZUNGUKA SOKO LA KARIAKOO.

DAWASA, JIJI, TARURA WAZIBUA MITARO YA MAJI TAKA INAYOZUNGUKA SOKO LA KARIAKOO.
Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA), Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) na Halmashauri ya Jiji ya Dar es Salaam wameshirikiana kuzibua mitaro ya maji taka inayozunguka Soko Kuu la Kariakoo. Akizungumza baada ya zoezi la uzibuaji wa mitaro hiyo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim amesema zoezi hilo linafanyika kufuatia maelekezo aliyoyatoa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo kuwa taasisi hizo zikutane na kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo na kuondoa kero kwa wananchi. CPA. Abdukarim amemshukuru na kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya na wakuu wa taasisi hizo kwa namna waliyoshughulikia changamoto hiyo na kutuma wataalam wao kufika katika maeneo hayo, kitendo ambacho kwa pamoja kimefanikisha kutekelezeka kwa maagizo ya Mhe. Mkuu wa Wilaya. Amesema shirika litaendelea kushirikiana na mamlaka hizo kuhakikisha kuwa maeneo yanayolizunguka soko…