UFUGAJI WA KISASA AJENDA KUU MAONYESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA.
UFUGAJI WA KISASA AJENDA KUU MAONYESHO YA MIFUGO KANDA YA ZIWA.
Wafugaji nchini wametakiwa kuachana na mbinu za jadi za ufugaji ambazo zimepitwa na wakati na badala yake kutumia teknolojia za kisasa za kidigitali zinazorahisisha usimamizi na ufuatiliaji wa mifugo kuanzia inapozaliwa hadi hatua ya kuchinjwa. Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Climb Up Limited, Emmanuel Ngallah, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Maonyesho ya Mifugo Kanda ya Ziwa Mei 30, 2026, mkoani Shinyanga. Ngallah alisema matumizi ya mifumo ya kidigitali katika sekta ya mifugo yanawawezesha wafugaji kupata taarifa sahihi kuhusu afya, ukuaji na historia ya mifugo yao, jambo linaloongeza tija na thamani ya biashara ya mifugo. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Agnes Meena mgeni rasmi katika maonyesho hayo, alisisitiza umuhimu wa wafugaji kuendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuongeza uzalishaji na kuifanya sekta ya mifugo kuwa na mchango mkubwa zaidi katika uchumi wa nchi. Alieleza kuwa serikali inaendelea kuhamasisha m…