DKT. MWIGULU: ACHENI UBOSI KWENYE KAZI ZA WATU
*Kijana Gideon amshukuru kurejeshewa fedha za mtaji wa dagaa WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka watendaji wa Serikali waache kufanya ubosi kwenye kazi za watu na pia waziheshimu kazi zao. "Lazima tuheshimu kazi za watu, tuheshimu jitihada za kila mmoja na tusifanye ubosi kwenye kazi za watu," alisema. Waziri Mkuu alitoa wito huo jana jioni (Jumamosi, Mei 23, 2026) wakati akizungumza na wakazi wa Iringa mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kichangani, Kihesa, nje kidogo ya Manispaa ya Iringa. Sambamba na wito huo, Waziri Mkuu alimwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Heri James awape maelekezo watumishi waliopo kwenye Halmashauri zote za mkoa huo na kuwataka waache kukamata vitendea kazi vya wananchi. "Mkuu wa Mkoa watangazie viongozi wa Halmashauri zote za mkoa wako wasikamate vitendea kazi vya wananchi. Sitaki kusikia sahani wala bakuli ya mama lishe imekamatwa," alisema na kuonya kuwa endapo vitendea kazi hivyo vimehusika na kazi za uhali…