Posts

CRDB YARAHISISHA UPATIKANAJI WA MIKOPO KWA WAFUGAJI

CRDB YARAHISISHA UPATIKANAJI WA MIKOPO KWA WAFUGAJI
Wafugaji nchini wameendelea kunufaika na huduma za kifedha baada ya kuongezeka kwa uelewa wao kuhusu masuala ya fedha na uwekezaji, hatua iliyowezesha kurahisishwa kwa vigezo vya dhamana ya kupata mikopo  kwa kutumia rasilimali walizonazo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Mifugo Kanda ya Ziwa, Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Anselem Mwenda, amesema benki hiyo imefanikiwa kuwasaidia wafugaji wengi kupata mikopo kwa urahisi kupitia huduma mbalimbali ikiwemo bima ya mifugo. Mwenda alitoa kauli hiyo mara baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Agnes Meena, kutembelea banda la CRDB, ambao ni wadhamini wakuu wa maonyesho hayo. Alisema kuwa kwa sasa wafugaji wana uwezo wa kukopesheka kwa urahisi zaidi kutokana na kuwa na bima ya mifugo pamoja na kutambuliwa kwa rasilimali zao kama sehemu ya dhamana. “Uelewa wa wafugaji umeongezeka kwa kiwango kikubwa tofauti na ilivyokuwa zamani. Hii imewasaidia kutumia fursa za kifedha zinazotolewa na benki kwa maen…