BAADA YA KIGOGO - BUSISI: SERIKALI KULETA NURU KISORYA - UKEREWE
BAADA YA KIGOGO - BUSISI: SERIKALI KULETA NURU KISORYA - UKEREWE
Kwa miongo kadhaa, wananchi wa Jimbo la Ukerewe wamepata changamoto kubwa ya kukosa mawasiliano ya usafiri hasa nyakati za usiku, hali ambayo imechochea kudhoofika kwa uchumi wa wananchi wa maeneo hayo kwa kukosa fursa za mwingiliano wa kibiashara na wilaya na mikoa jirani. Kwa kutambua changamoto hiyo, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia bajeti ya Wizara ya Ujenzi iliyowasilishwa Mei 21, 2026 na Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Mhe. Abdallah Hamis Ulega, bunge lilipitisha shilingi trilioni 2.564 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ndani yake ikiwepo ujenzi wa daraja jipya linalounganisha Ukerewe - Kisorya, Bunda. Hatua hiyo imeibua hisia zilizojaa furaha kwa wananchi wa jimbo hilo ambao kwa miongo kadhaa walijiona kuwa kifungoni kwa kutokuwepo na miundombinu ya daraja katika kivuko cha Kisorya - Ukerewe hali iliyochochea kukosekana kwa mawasiliano kati ya Ukerewe na mikoa jilani. Katika bajeti hiyo, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi inayosima…