TIRDO YAWAALIKA WADAU WA NGOZI KUPATA UTAALAM WA UZALISHAJI BORA

TIRDO YAWAALIKA WADAU WA NGOZI KUPATA UTAALAM WA UZALISHAJI BORA
Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) imewaalika wadau wa ngozi nchini kupata mafunzo juu ya uchakataji na utengenezaji bidhaa za ngozi nchini . Hayo yameelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa TIRDO Mhandisi Ramson Mwilangali wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa wanafunzi na wazalishaji wa Bidhaa za ngozi nchini . Mafunzo hayo ya siku tano yamelenga kuwajengea uwezo wazalishaji wa ngozi kutoka mikoa ya Pwani , Morogoro,Dar es salaam na Kilimanjaro lengo likiwa ni kuhakikisha ngozi inayozalishwa hapa nchini inachakatwa na kuzalisha bidhaa tofauti na sasa ambapo kwa kiasi kikubwa ngozi inauzwa nje ya nchi kabla ya kuchakatwa . Mhandisi Ramso amesema kuwa soko la Tanzania inahitaji zaidi ya jozi ya viatu milioni 54 huku Viwanda vya ndani vikizalisha jozi elfu tatu tu ambayo ni chini ya asilimia kumi ya mahitaji bidhaa hiyo kwa mwaka. "Tunalenga kuongeza uzalishaji wa ndani kufikia asilimia 50 ya mahitaji ya nchi ili kuziba pengo linaloagizwa kutoka nje . Kwa upande wa m…