Kutembelea wagonjwa ni fursa ya kuelewa shida za wananchi - OMO
Kutembelea wagonjwa ni fursa ya kuelewa shida za wananchi - OMO
Mwenyekiti
wa Taifa wa chama cha ACT Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema kwamba
ziara za kuwatembelea wagonjwa na wenye shida katika kipindi cha mwezi mtufufu
wa ramadhani ni fursa muhimu kwa viongozi kutambua kwamba wanadhamana kubwa kwa
wananchi kuzielewa shida na matatizo waliyonayo na kutafuta namna sahihi ya
kuyakabili. Mhe. Othman
ameyasema hayo huko Milimani Kiembe Samaki wilya ya Magharib B alipofanya
majumuisho baada ya kukamilisha ziara ya kutembelea wagonjwa ndani ya Wilaya ya
Magharib A na B akiwa katika siku ya tatu ya mfululizo wa ziara zake za aina
hiyo katika kisiwa cha Unguja. Mhe. Othman
ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mstaafu, amesema kwamba wananchi
wanayo matatizo na shida nyingi ambapo kupitia ziara kama hizo viongozi
wataweza kuzitambua kwa urahisi kwa kufika mwenyewe kwenye maeneo yao
wanayoishi wananchi. Amesema ndani ya kipindi cha miaka mitano yakuendeleza
ziara hizo amepata uzoefu mkubwa pamoja na kujifunza mambo mengi kutoka kwa
wan…